Responsive image
  1. UTANGULIZI.

    Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Mjini Mtwara (MTUWASA) chini ya Bodi ya Wakurugenzi ilianzishwa rasmi tarehe 01/01/1998 kwa sharia ya Maji Ma. 8 (Water Works ordinance Cap 281) ya mwaka 2007 ambayo imerebishwa na sheria Na. 12 ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Mwaka 2009. Mtuwasa sasa ina umri wa miaka kumi na saba (17) tangu kuanzishwa kwake. Jukumu la msingi la MTUWASA ni kutoa huduma bora na endelevu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira katika Manispaa ya Mtwara/Mikindani.

  2. DHUMUNI LA MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA.

    Dhumuni la Mkataba huu ni kuweka bayana huduma zinazotolewa na MTUWASA, na viwango vya huduma hizo, ambazo wateja na wadau wana haki ya kufahamu, lakini pia dhumuni jingine kueleza Dira ya Mamlaka, dhamira, haki na wajibu wa Mamlaka na wateja kwa ujumla.

  3. DIRA YETU (VISION).

    Kuwa mamlaka inavyoongoza katika kutoa huduma bora na endelevu ya Majisafi na usafi wa mazingira nchini Tanzania.

  4. DHAMIRA YETU (MISSION).

    Kutoa huduma bora ya Majisafi na salama pamoja na uondoaji wa Majitaka katika mji wa Mtwara Mikindani.

  5. WATEJA WETU.

    Mamlaka yetu ina Wateja na wadau muhimu kama ifuatavyo:

    • Wateja (Watumiaji wa Majumbani, Wafanyabiashara, Taasis, Viwandani, Viosk na umma wote kwa ujumla.)
    • Watumishi.
    • Wafadhili.
    • Serekali kuu na Halimashauri ya Manispaa.
    • Wanasiasa.
    • Vyombo vya Habari
    • Mashirika yasiyo ya kiserikali

  6. HAKI NA WAJIBU WA MTEJA.

    • Kupata huduma ya Majisafi na Salama.
    • Kupata taarifa muhimu zinazohusu huduma zetu.
    • Kuhudumiwa kirafiki na kwa usawa.
    • Kutoa malalamiko na maoni
    • Kulinda dira (mita) ya maji.
    • Kilipa anakara ya maji kwa wakati.
    • Kutoa taarifa zote zinahusiana na wizi wa maji na mivujo ya maji.
    • Kushirikana na watumishi wa Mamlaka pale wanapofanya shighuli yoyoyte inayohusiana na huduma zetu.

  7. HAKI NA WAJIBU WA MTUWASA.

    • Kuzalisha na kusambaza majisafi na salama kwa Viwango vinavokubalika.
    • Kufanya upanuzi na matengenezo ya miundo mbinu ya majisafi.
    • Kutayarisha ankara sahihi za majisafi na kuzisambaza kwa wateja.
    • Kukusanya maduhuli.
    • Kuajiri watumishi waadilifu.
    • Kushughulikia malalamiko na matitizo ya wateja na wadau haraka iwezekanavyo.
    • Kusitisha huduma ya majisafi kwa mteja pale anapokiuka sheria na taratibu za Mamlaka.
    • Kuwahamasisha na kuwaelimisha wateja juu ya utumiaji bora wa Maji na utunzaji wa rasilimali za maji hasa Vyanzo vya Maji.

  8. HUDUMA ZINAZOTOLEWA KWA MTEJA.

    • Maunganisho Mapya ya Maji.
    • Urejeshaji wa huduma ya maji yaliyositishwa.
    • Uzibaji wa mivujo.
    • Usomaji wa dira (mita)nza wateja.
    • Usitishaji wa huduma kwa hiari.
    • Urekebishaji wa ankara za Maji.
    • Utoaji wa ankara za Maji.
    • Ubadilishaji kwa taarifa za mteja.
    • Ulipaji wa ankara za Maji.

  9. TARATIBU ZA MAUNGANISHO MAPYA.

    • Mteja anatakiwa kujaza fomu ya maombi na kuirudisha MTUWASA.
    • Idara inayohusika inatakiwa kwenda kuona eneo la mteja na kuandaa gharama za mteja ndani ya siku mbili baada ya malipo.
    • Maunganisho ya huduma na uwekaji wa dira unatakiwa ufanyike ndani ya siku saba baada ya malipo ya gharama zote.
    • Malipo ya Gharama za Maunganisho mapya yanafanyika Ofisi kuu ya MTUWASA tu na sio kwenyeviyuo vyetu vya malipo.

  10. MALALAMIKO, MAULIZO NA MAON YA MTEJA.

    Tunapokea na kujibu malalamiko yote, malalamiko yaliyowasilishwa kwa maandishi yatajibiwa ndani ya siku sita za kazi. Jumatatu hadi jumamosi. Tunapokea maoni katika sanduku letu la maoni na tunathamini usiri wa maoni ya mteja.

  11. NAMNA YA KUTUMA MALALAMIKO YAKO

    Malalamiko, Maoni na Maombi yote yatumwekwa anuani ifuatayo.


MKURUGENZI MTENDAJI,
MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA,
SLP 141,
MTWARA

Laravel