Responsive image

New connection

 1. Mteja atajaza fomu ya maombi ya kuunganishiwa huduma ya maji. Fomu zinapatikana Jengo la huduma kwa wateja bila malipo yoyote fomu hiyo inaambatanishwa na nakala ya kitambulisho cha uraia,leseni ya udereva au kitambulisho cha mpiga kura

 2. Wataalam wa mamlaka watafanya ukaguzi(survey) kwenye eneo/nyumba inayoombewa huduma ya maji na kutayarisha gharama

 3. Mteja atapata taarifa ya ukaguzi na gharama za kuungiwa maji baada ya siku saba kuanzia tarehe aliyojaza fomu ya maombi ya huduma.Taarifa hizi atazipata kwa kupigiwa simu au kwa kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno kwamba gharama zako zipo tayari.

 4. Mteja atafika ofisini kuchukua nyaraka halisi za maunganisho mapya na kupatiwa control namba kwa ajili ya malipo

 5. Gharama zote zitalipwa kwa mamlaka kupitia mitandao ya simu, benki au kwa mawakala wa benki na mteja atapata stakabadhi ya kieletroniki na kivuli chake kama kuna uihataji inayolingana na malipo atakayofanya.

 6. Baada ya malipo mteja ataacha kivuli cha nakala ya nyaraka zote za maunganisho mapya kwa ajili ya kumbukumbu.


 1. Gharama za mabomba na viungio vinavyohitajika kuanzia bomba kuu hadi kufika katika eneo / kiwanja cha mteja

 2. Gharama za kuchimba na kufukia mtaro wa bomba.

 3. Gharama za usimamizi (supervision charge)

 4. Gharama za uwakala (agency fees-20%)


 • Endapo mteja atafanya malipo atastahili kupata huduma hiyo ndani ya siku saba kuanzia tarehe atakayokuwa amefanya malipo.

 • Iwapo kutakuwa na sababu zisizozuilika zitakazofanya mteja asipatiwe huduma katika muda uliopangwa ,Mamlaka itampa mteja taarifa rasmi.

 • Endapo mteja hatakuwa ameridhaika na huduma atakayopewa ana haki ya kuwasilisha maoni yake kwa Afisa Huduma kwa wateja.

Laravel